Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura katika kikao cha dharura kilichofanyika March 2, 2022 ili kupitisha Azimio la kulaani hatua ya kijeshi ya Urusi dhidi ya Ukraine.

Aidha azimio hilo limepitishwa kwa kura 141 zilizokubali azimio, kura 35 hazikuunga mkonona kura Tano tu zikiwa dhidi yake.

UN imesema kuwa vita hivyo vinavyoendelea ilikuwa ni kama chaguo la mtu mmoja ambaye ni Rais Putin na kufanya watu kukimbia nchi Yao na kupelekea hata watoto waliokuwa katika matibabu mbalimbali kukatisha matibabu Yao ikiwemo watoto wenye saratani.

“Kuwafanya watoto walio na saratani kukusanyika katika vyumba vya chini vya hospitali, kukatiza matibabu yao, kimsingi kuwahukumu kifo. Hayo yalikuwa chaguo la Rais Putin. Sasa ni wakati wa sisi kufanya yetu,” Amesema Balozi wa Marekani, Linda Thomas-Greenfield

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia wanadiplomasia ujumbe wa Baraza Kuu “ni mkubwa na wazi na kumtaka Putin kumaliza uhasama dhidi ya Ukraine na kungua milango ya mazungumzo wa kidiplomasia.

Naye Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Amesema kuwa wale waliounga mkono azimio hilo wamechagua sehemu sahihi katika historia.

Kanye na Kim ndio basi tena
Serikali yajipanga kutokomeza Malaria 2030