Diana Bundala maarufu Zumaridi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mwanza, kwa tuhuma za makosa matatu ambapo kesi ya kwanza ni Kesi namba 10 ya mwaka 2022 ,inayomkabili Zumaridi na wenzake 8 ambayo ni Shambulio la kuzuru mwili pamoja na kuzuia watumishi wa umma ambao ni askari kufanya kazi yao.

Shtaka lingine linalomkabili Zumaridi ni Kesi namba 11 ya mwaka 2022, ambapo Zumaridi anatuhumiwa kwa kosa la usafirishaji wa Binadamu.

Zumaridi pia anatuhumiwa kwa kosa la tatu akiwemo yeye na wenzake 84 ambapo ni kesi namba 12 ya mwaka 2022, kwa tuhuma za kufanya kusanyiko lisilo halali, pamoja na tuhuma za kushambulia Mwili.

Afariki akifanya tendo la ndoa
Wakamatwa kwa kukutwa na nyara za serikali