Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy ameikosoa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi ((NATO) akieleza kuwa ilikataa ombi lake la kulifunga anga la nchi hiyo (no-fly zone) kuepuka mashambulizi ya anga.

Akizungumza katika hotuba yake kwa dunia, Rais Zelenskyy alisema kuwa NATO walikataa ombi hilo wakifahamu kuwa Urusi ingeweza kuishambulia Ukraine muda wowote, kitendo alichosema ni kama kutoa ruhusa kwa Urusi.

“Wakifahamu kuwa mashambulizi hayaeupukiki, NATO waliamua kwa makusudi kukataa kufunga anga la Ukraine,” alisema Zelenskyy.

“Leo viongozi wa umoja huu wametoa ruhusa kwa mashambulizi zaidi dhidi ya majiji ya Ukraine na vijiji vyake, kwa kukataa kuweka zuio la kupita kwenye anga la Ukraine,” aliongeza.

Urusi imeendelea kuishambulia Ukraine licha ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kijamii na mataifa yanayoiunga mkono nchi hiyo.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameendelea kutoa wito kwa majeshi ya Ukraine kuweka silaha chini au kuipundua Serikali ya nchi hiyo, huku wakiendelea kudhibiti baadhi ya miji muhimu.

Putin amefungua milango kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo, lakini Zelenskyy amemtaka kusitisha kwanza mashambulizi.

Kenya: Mgombea urais ajitoa, atangaza kumuunga mkono mpinzani
Fursa mpya kwa vijana zatangazwa