Kiungo Mshambulaiji kutoka Burundi na klabu ya Young Africans Saido Ntibazonkiza ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Februari 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ leo Jumapili (Machi 06), Kiungo huyo aliyebahatika kucheza soka Barani Ulaya (Uholanzi na Ufaransa) ametangazwa kuwa mshindi wa Kinyang’anyiro hicho akiwashinda Fistoni Mayele wa Young Africans na Reliant Lusajo wa Namungo FC.

Saido anakua mchezaji wa sita kutwaa tuzo hiyo msimu huu, akitanguliwa na Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania), Feisal Salum (Young Africans), Jeremiah Juma (TZ Prisons), Reliant Lusajo (Namungo FC) na Fiston Mayele (Young Africans).

Sababu za Saido kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Februari zilizotolewa kwenye taarifa ya TPLB, ameisaidia klabu yake ya Young Africans kupata ushindi kwenye michezo miwili na sare moja huku akionesha kiwango kizuri na kufunga mabao mawili, huku akihusika katika mabao mengine matatu.

Nasreddine Nabi tishilo Ligi Kuu Bara
Mwinyi Zahera: Mayele ashindwe yeye tu!