Mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji FC uliokua umepangwa kuanza saa moja usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa, umefanyiwa mabadiliko ya muda na sasa utaanza mishale ya saa kumi jioni.

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam kesho Jumatatu (Macho 07), huku ikiwa na matarajio ya kuziwania alama tatu muhimu za mtanange huo.

Meneja wa Habari wa Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ametoa taarifa za mabadiliko hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ‘FACEBOOK’ kwa kuandika: MABADILIKO YA MUDA WA MCHEZO. 

Mechi yetu ya kesho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji ambayo awali ilikuwa ichezwe saa moja usiku, sasa itapigwa saa 10 jioni.

Tayari uongozi wa klabu umepokea taarifa ya maandishi kutoka Bodi ya Ligi kuhusu mabadiliko hayo ya muda wa mchezo.

Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri kila kitu kipo kama kilivyopangwa na kinachosubiriwa ni muda tu ufike mchezo huo upigwe tuendelee ku enjoy.

Habari Picha: Rais Mwinyi akutana na viongozi wa mifuko ya jamii
Ssetuba: Chama, Sakho sio watu wazuri