Jeshi la Polisi mkoani Tabora limesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini bado litaendelea kutekeleza mpango mkakati wake wa kupunguza matukio ya uhalifu hususani mauaji ya mara kwa mara ambayo chanzo chake ni wivu wa kimapenzi, kuwania mali na dhana potofu ya ushirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP, Richard Abwao katika taarifa yake aliyoitoa wakati wa Sherehe za Siku ya Polisi na familia iliyofanyika leo Machi 6, 2022 mjini Tabora, amekiri kwamba wamefanikiwa kupunguza makosa ya jinai kwa asilimia 7.2 kwa mwaka 2020 huku makosa makubwa ya jinai nayo yakipungua kwa asilimia 5.6 kutoka mwaka 2020 hadi 2021.

Akikabidhi zawadi kwa askari 16 waliofanya vizuri kwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kukataa kupokea rushwa kutoka wa wahalifu, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Buriani ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulipa ushirikiano Jeshi hilo la Polisi katika kukabiliana na matukio ya uhalifu hususani mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kuchafua sifa ya Mkoa wa Tabora.

Mayele aipa jeuri Young Africans
Raia 17 kutoka Ethiopia wakamatwa