Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amepongeza maonyesho ya wafanyabiashara wanawake yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri Jafo aliyasema jijini Dar es Salaam wakati akifungua maonyesho hayo ambayo yanaendelea kwenye viwanja hivyo ambayo yanatarajiwa kufikia kilele siku ya Alhamisi kwa wanawake mbalimbali kupewa tuzo.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake (TWCC)  na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ na wafadhili mbalimbali.

 Akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo jijini  Dar es Salaam, Waziri Jafo amesema baada ya kutembelea mabanda mbalimbali amejionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wafanyabiashara wanawake ambazo nyingi zinaviwango vya kimataifa.

Simba SC Vs Dodoma Jiji yarudishwa saa Moja
Simba, Dodoma Jiji zapokea taarifa ya TPLB