Mtahiniwa mmoja wa Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE) katika kaunti ya Kisii nchini Kenya anafanya mtihani huo katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii (KTRH) baada ya kujifungua siku moja kabla ya mtihani huo.

Haya yamethibitishwa na Katibu Mkuu wa Elimu, Julius Jwan ambaye alizungumza baada ya kushuhudia kufunguliwa na kusambazwa kwa mtihani huo kutoka kaunti ndogo ya Kisii ya Kati hadi vituo vya mitihani.

Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) watahiniwa 1,225,507 wanafanya mtihani huo katika vituo 28,316 ikilinganishwa na mwaka 2020 ambapo watahiniwa walikuwa 1,191,752 katika vituo 28,467.

Kwa mujibu wa agizo la Wizara ya Elimu, ni manaibu makamishna wa Kaunti (DCC) na Kamishna Wasaidizi wa Kaunti (ACC) ambao wanaruhusiwa kufungua na kufunga mashehena ya mitihani katika Kaunti Ndogo zao na Mitihani yote inasafirishwa kutumia magari ya serikali na kwa ulinzi wa angalau afisa mmoja wa polisi.

Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC) watahiniwa 1,225,507 wanafanya mtihani huo katika vituo 28,316 ikilinganishwa na mwaka 2020 ambapo watahiniwa walikuwa 1,191,752 katika vituo 28,467.

Mameneja wa vituo watashirikiana na maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa hakuna kataratasi au maswali yanafikia watahiniwa kabla ya muda rasmi wa karatasi hilo kufanywa.

Waziri wa Usalama Fred Mataing’i na baadhi ya watahiniwa wa mtihani wa KCSE

Maafisa mbalimbali wa serikali wakiwemo mawaziri na makatibu wamejitokeza kwa uangalizi wa mwanzo wa zoezi hilo hii leo wakiongozwa waziri wa Elimu George Magoha na mwenzake wa Usalama Fred Matiang’i.

Mtihani ya kitaifa ya darasa la nane (KCPE) imeng’oa nanga hii leo nchini Kenya Jumatatu, Machi 7 ikitarajiwa kukamilika Machi 9.

Kikwete: Serikali ya Rais Samia ukiibipu inakupigia
Putin aiamuru Ukraine kuinua mikono