Licha ya umahiri pamoja na mafanikio yake makubwa kwenye muziki na biashara mbali mbali, nyuma ya pazia, rapa Dizz Drake ni mpenzi mkubwa wa michezo ya kubashiri.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika inaelezwa siku takriban tatu zilizopita rapa huyo kutoka nchini Canada aliliwa kiasi cha pesa zaidi ya Tsh milioni 645 za Kitanzania.

Hii ilikuwa katika ubashiri wa pambano la UFC ambapo Drake alielekeza ushindi kwa Masvidal ambaye mpaka mwisho wa mchezo aliishia kuchezea kichapo cha Covington.

Taarifa zinasema kabla ya uchungu wa mamilioni aliyoliwa haujapotea, Colby Covington alimrushia maneno rapa huyo akimtaka aachane na masuala ya kubashiri (betting) na ajikite katika kufanya biashara ya album zake alizoziita za kipuuzi.

Tiba ya macho yasogezwa kwa jamii
Ali Kiba ampongeza Khaligraph Jones ujio wa Invisible Currency