Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin anaamini bado kikosi chake kina nafasi ya kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo msimu huu 2021/22.

Pablo ameonesha imani hiyo, baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu uliounguruma jana Jumatatu (Machi 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema anaamini ubingwa bado upo wazi, na kikosi chake kina nafasi ya kutetea ubingwa wake, hivyo lolote linaweza kutoka.

” Kwa namna msimu huu ulivyo naamini hilo linawezekana licha ya kuwa nyuma kwa pointi kadhaa. Ninawaamini wachezaji wangu, kama ambavyo tulishindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi na kuachwa pointi hizo, wapinzani wetu nao linaweza kuwatokea jambo kama hilo.” amesema Kocha Pablo.

Simba SC imefikisha alama 37 ikiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitanguliwa na Young Africans iliyo kileleni kwa kumiliki alama 45.

Samatta kuibeba Twiga Stars
RS Berkane wampa kazi maalum Kocha Ibenge