Mrembo mmoja raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 24, anayejulikana kwa jina Teresia, amefichua kuwa yeye huchumbiana na wanaume wote ambao hugharamia maisha yake ya kifahari.

Akizungumza katika mahojiano na mchungaji Jimmy Kay, Teresia alisema huwatosheleza wanaume hao wote kingono na huvuna zaidi ya shilingi TSh milioni 1,200,000 kutoka kwa kila mmoja wao na ameweka kwa mtu yeyote ambaye anachumbiana naye au anayetaka kumchumbia.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 24, alifichua kuwa kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume sita ambao wameoa.

Teresia alisema kuwa wanaume wenyewe ndio humtafuta na yeye hawatafuti na alipoulizwa umri wa wapenzi wake alisema ni kuanzia miaka 53.

Katika taarifa sawia na hiyo, Pasta Jimmy Kay ambaye alimuhoji binti huyo alionya kuwa wanaume wasiojiweza kifedha hawatakiwi kuoa.

“Usiwahi kufikiria kuibua suala la ndoa kama wewe ni mvulana. Waachie watu walio na msimamo wa kifedha na waliokomaa. Itakuvunja. Unaweza kuingia kwenye ndoa ukidhani anakupenda. Hii ni moja ya sababu kwa nini kuna visa vingi vya talaka kwa sababu ndoa imekiukwa,” alisema.

Matamshi hayo ya Jimmy yalizua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wao wakikutana wakimzomea wakidai anawapotosha wanawake.

?rane: Hakuna asiyependa kufanya kazi Simba SC
Pablo: Jukumu la penati nimemkabidhi Chama