Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 9 hadi 12 Machi 2022.

Ziara hiyo inafuatia mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021. 

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika kikao cha paamoja na timu aliyoambatana  nayo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kujipanga kwa pamoja wakati wa ziara ya kikazi nchini humo mara baada ya kuwasili.  Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  akimsikiliza.

Akiwa nchini Saudi Arabia Waziri Mulamula anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi,  viongozi wengine wanaosimamia sekta za sekta za Mifugo na Utalii na wafanyabiashara  na wenye viwanda wa Saudi Arabia.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania mjini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah..

Balozi Mulamula na ujumbe wake watarejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

Waratibu tiba asili wapewa jukumu na serikali
Kocha Azam FC awavaa wachambuzi