Mtu wa kwanza kupandikizwa moyo wa nguruwe amefariki dunia miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Maryland.

Hospitali hiyo ilitangaza Jumatano, Machi 9, kuwa David Bennett, 57, alikata roho mnamo Jumanne, Machi 8, katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Maryland.

Kulingana na madaktari wake, hali ya afya ya Bennett ilianza kuzorota na kuwa mbaya siku kadhaa zilizopita.

“Alionekana kuwa mgonjwa jasiri na mzuri ambaye alipigana hadi mwisho,” alisema daktari aliyemfanyia upandikizaji huo Bartley Griffith.

Bennett, ambaye alikuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza moyo huo mnamo Januari 7 na upandikizaji huo unadaiwa ndio ulikuwa njia pekee ya matumaini ya kuokoa maisha ya Bennett ikiwa wakati huo madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba Bennet angelipoteza maisha yake.

Mwanaume huyo alikuwa akionekana hakuwa na uwezo wa kupandikizwa moyo wa binadamu, uamuazi ambao huchukuliwa na madaktari wakati afya ya mgonjwa inapozorota zaidi.

Nguruwe aliyetumiwa katika upandikizaji huo alifanyiwa mabadiliko ya vinasaba ili kuondoa jeni kadhaa ambazo zingefanya kiungo hicho kikataliwe na mwili wa Bennet.

Hata hivyo Madaktari waliofanya upandikizaji huo, walisema endapo yangekuwa ni mafanikio yangehitimisha miaka kadhaa ya utafiti na kubadili maisha kote duniani na ni hatua moja ya kukaribia kutatua mzozo wa ukosefu wa kiungo cha mwili.

Katika majaribio ya awali ya upandikizaji kama huo yalishindikana kwa kiasi kikubwa kwa sababu miili ya wagonjwa ilikataa kiungo cha wanyama haraka.

Wanawake Afrika hatarini zaidi kuugua Ugojwa wa Figo
Kenya kuachana na uvaaji wa barakoa