Wakati mataifa mengi ya Magharibi yakitaka kuitenga Urusi baada ya kuivamia Ukraine, wataalam wanasema Moscow inakuza uhusiano na mshirika wake wa muda mrefu wa Kiafrika, Sudan, ikiendelea kujikaribisha na utajiri wake wa dhahabu.

Watalamu wa masuala ya kimataifa wanasema kuwa Khartoum imepoteza uungwaji mkono na mataifa ya Magharibi tangu mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan alipoongoza mapinduzi ya kijeshi Oktoba mwaka jana, hatua iliyozua shutuma kubwa ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa msaada wa dola milioni 700 za Marekani.

Mnamo Februari 23, siku moja kabla ya Urusi kuvamia jirani yake Ukraine, wajumbe wa Sudan wakiongozwa na kamanda jeshi Mohamed Hamdan Daglo waliwasili Moscow Urusi, kwa ziara ya siku nane na pande hizo mbili zilijadili mada za kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, pamoja na usalama wa kitaifa wa Urusi na Sudan ikiwemo ushirikiano wa pamoja na kukabiliana na ugaidi,” alisema Daglo, katika mkutano na waandishi wa habari aliporejea.

Sudan iliitegemea kijeshi Urusi chini ya kiongozi shupavu Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani mwaka 2019 baada ya kuongoza kwa miongo mitatu ambapo serikali yake ilitengwa kimataifa na kulemazwa vikwazo vya Marekani.

Hata hivyo kampuni za kibinafsi za Urusi zimeripotiwa kufaidika na migodi ya dhahabu ya Sudan kwa kuimarisha uhusiano na wanajeshi na Vikosi vya Msaada vya Haraka vya Daglo, ambavyo viliibuka kutoka kwa wanamgambo wa Janjaweed wanaotuhumiwa kwa ukatili wakati wa mzozo wa Darfur uliozuka mnamo 2003.

“Moscow imekuwa ikifuata sera iliyo wazi na thabiti na kutumikia maslahi yake, nchini Sudan na barani Afrika kwa mapana zaidi, Uwekezaji wa Urusi nchini Sudan, hasa katika dhahabu, na uhusiano na vikosi vya usalama umesalia kugubikwa na sintofahamu,”mchambuzi Khaled al-Tijani.

Mtafiti Ahmed Hussein alisema kuwa kuna uwezekano Daglo alijadiliana huko Moscow kuhusu mipango kati ya vikosi vyake na “vyombo vya ulinzi vya Kirusi (vya usalama) vyenye uhusiano nchini Sudan na Afrika, hasa Wagner Group.”

Wagner, mkandarasi wa kijeshi wa kibinafsi wa Urusi na uhusiano na Kremlin, amekabiliwa na shutuma za kuhusika katika machafuko na majirani za Sudan Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya, wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwezi uliopita alionya juu ya nia ya uporaji ya kikundi hicho nchini Mali.

Baraza la Ulaya la Mahusiano ya Kigeni limesema wafanyakazi wa Wagner walitumwa nchini Sudan kwenye maeneo ya uchimbaji madini kufuatia mkutano wa 2017 kati ya Bashir na Rais wa Urusi Putin, ambao walikubaliana mikataba ya uchimbaji madini ya dhahabu na kujadiliana kuhusu ujenzi wa kituo cha jeshi la wanamaji la Urusi kwenye Bahari Nyekundu ya Sudan.

Wafanyakazi wa Wagner baadaye walitoa msaada mbalimbali wa kisiasa na kijeshi kwa utawala wa Bashir, kulingana na ECFR, Pia katika mwaka wa 2017, kampuni ya uchimbaji madini ya Urusi ya M-Invest ilikubalika katika hifadhi ya dhahabu ya Sudan, kulingana na Carnegie Endowment for International Peace.

Miaka mitatu baadaye, Marekani iliweka vikwazo kwa oligarch wa Urusi Yevgeny Prigozhin, ambaye ana uhusiano na M-Invest na anaaminika kuwa anamiliki Wagner, kwa kuaminika kuwa ananyonya maliasili ya Sudan kwa manufaa ya kibinafsi na kueneza ushawishi mbaya kote ulimwenguni.

ECFR ilisema Wagner alikuwa ameunda pembetatu ya ushawishi wa Urusi inayounganisha Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya, ikionyesha nia ya kimkakati ya Moscow katika kupanua nyayo zake za Afrika.

Taarifa za ndani na za uhakika zinasema kuhusu kambi ya wanamaji iliyopangwa katika mji wa kimkakati wa Port Sudan, Warusi wanahitaji kufika kwenye bandari za maji ya joto, na Bahari Nyekundu ni sehemu muhimu ya matarajio hayo.

Wataalamu wa Ugavi 230 watakiwa kurudia mitihani ya kitaaluma
Urusi yakanusha kulipua Hospitali ya watoto