Meneja wa klabu ya Aston Villa, Steven Gerrard amesema hana haraka ya kumsajili kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho Correia aliyemsajili kwa mkopo Mwezi Januari akitokea FC Barcelona.

Coutinho alisajiliwa klabuni hapo baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha FC Barcelona chini ya Meneja mpya Xavier Hernández Creus.

Gerrard amelazimika kutoa kauli ya kutokua na haraka ya kusajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, kufuatia mkataba wake wa uhamisho wa mkopo, kuwa na kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja endapo Aston Villa itaridhishwa na kiwango chake.

Hata hivyo klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya England italazimika kutoa Pauni Milioni 33 kama ada ya uhamisho wa Coutinho.

Gerrard amesema: “Kwa sasa kiwango chake ni kama kile cha zamani akiwa Liverpool.”

“Kwangu haileti maana kufanya uamuzi wowote kwa sasa, tunahitaji kumfanya afurahie hapa.”

“Kumweka sawa mpaka mwisho wa msimu na nina uhakika atatusaidia sana, kumwangalia na kufanya nae kazi na kumwona akirudi kwenye kiwango chake huku akifurahia mpira wake tena.”

Xavi afichua siri ya kuwanasa wachezaji FC Barcelona
Kisinda aitahadharisha Simba SC