Vikosi vya Urusi vimeushambulia mji wa bandari wa Ukraine, Mariupol, huku wakaazi wakijificha katika msikiti wa kihistoria na kwingineko kuepuka milipuko. Mapigano pia yamepamba moto nje ya mji mkuu Kyiv, wakati Urusi ikiendeleza mashambulizi yake dhidi ya miji kote nchini Ukraine. 

Mji wa Mariupol umehimili mashambulizi makubwa kabisaa ya Ukraine tangu Urusi iivamie nchi hiyo Febrauri 24. 

Mashambulizi yasioisha yamekwamisha juhudi za kupeleka chakula, maji na dawa katika mji huo wa wakaazi laki nne na 30 elfu, na kuwaondoa raia wake waliokwama. 

Kwa mujibu wa ofisi ya meya wa mji huo, zaidi ya watu 1,500 wamekufa mjini Mariupol wakati wa mzingiro, na mashambulizi yamevuruga hata juhudi za kuwazika wafu katika makaburi ya watu wengi.

 Afisa wa serikali ya Ukraine alisema jana kuwa msikiti wa Sultan Suleiman ulipigwa, lakini vidio ya Instagram iliyowekwa na mwanaume aliedai kuwa rais wa chama cha msikiti huo, alisema ulinusurika baada ya bomu kuanguka umbali wa mita 700.

Dkt Gwajima akemea mauaji ya wazee
Moto wateketeza kiwanda cha GSM