Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amekemea vikali matukio ya mauaji ya wazee kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya Ushirikina ambapo Takwimu zinaonesha kupungua kwa matukio hayo kutoka vifo 190 mwaka 2015 hadi vifo 52 mwaka 2020.

Waziri Dkt. Gwajima amebainisha hayo Jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Baraza la kwanza la Taifa la Wazee ambapo amesema serikali bado inapambana kupunguza vifo vya wazee vitokanavyo na mila potofu.

Vilevile Waziri Dkt. Gwajima ameeleza juu ya nia ya serikali ya kuanzisha sheria mpya ya wazee inayotokana na sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003.

”Wale ambao wanapanga na kuendelea kuuawa wazee kwa kisingizio cha uchawi huu uchawi wanauonaga wao tuu kwamaba et mtu macho yake yakiwa menkundu et ndiyo uchawi”

”miaka sitini baada ya uhuru bado tunaongelea uchawi, ndiyo maana Mhe. Rais ametangeneza hii Wizara tutashuka mpaka kwenye jamii tukaangalie huo uchawi, mbona mnaua watu tumekuja kuyashughulikia hayo ambayo yamekuwa changamoto” amesema Waziri Gwajima

Urusi yashambulia kambi ya jeshi ya Ukraine iliyopo mji wa Lviv
Mashambulizi ya Urusi karibu na mji mkuu Kyiv