Katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express iliyotokea eneo la enjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, watu wanne wamefariki na wengine 35 wemejeruhiwa

Basi hilo ambalo lilikuwa linatoka Tunduma kwenda Dar es Salaam limepata ajali leo Jumatatu Machi 14, 2022 asubuhi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amesema kuwa watu hao wanne wamefariki dunia papohapo na wengine 35 wakijeruhiwa.

Kamanda Ngonyani amesema kuwa majeruhi wamefikishwa katika hospitali ya Vwawa kupata matibabu huku miili ya marehemu ikihifadhiwa hospitalini hapo.

“Basi hilo limetumbukia kwenye korongo baada kuviringika mara kadhaa na hatimaye bodi ya gari kukatika kuanzia kwenye usawa wa madirisha” amesema Ngonyani

Aidha amesema kuwa tarifa ya chanzo cha ajali hiyo itatolewa baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Mayele akabidhiwa Ng'ombe Dar
Chama awapongeza wachezaji Simba SC