Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Samwel Mhina (31) mkazi wa Temeke pamoja na wenzake 13 kwa tuhuma za kusambaza video katika mitandao ya kijamii kinyume na sheria.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Kamanda Muliro Jumanne amesema kuwa mara baada ya kusambaa kwa video hiyo wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na wafanyakazi wake walikuwa katika taharuki kubwa
Muliro amesema baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili kuhusishwa ililazimisha uchunguzi uanze mara moja ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilifanya uchunguzi huo.
Mhina ambaye ni mwandishi wa habari na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa U-Turn Collection na wenzake wanatuhumiwa kusambaza video hiyo ikimuonesha mgonjwa akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki zikiwemo kamera, kalama za kiuchunguzi (spying pens), miwani ya kichunguzi, kofia zenye kamera, laptop, memory cards.