Kikosi cha Simba SC kimewasili salama mjini Cotonou-Benin, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko watano wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Simba SC, kikosi cha Mabingwa hao wa Tanzania Bara kimewasili Cotonou-Benin saa tisa alasiri kwa saa za Afrika Mashariki kupitia Addis Ababa Ethiopia.

Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally aliwaambia waandishi wa habari kabla ya kuanza safari Jijini Dar es salaam mapema leo Ijumaa kuwa, Kikosi chao kitafanya mazoezi mepesi leo jioni mjini Cotonou-Benin, kabla ya kukamilisha Program maalum kesho Jumamosi (Machi 19), tayari kwa mchezo wa Jumapili (Machi 20).

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi D ikiwa na alama 07 baada ya kuifunga RS Berkane Jumapili (Machi 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, huku ASEC Mimosas ikiwa nafasi ya pili kwa ufikisha alama 06.

RS Berkane imefungana kwa alama na ASEC Mimosas lakini ipo nafasi ya tatu, huku USGN ikiburuza mkia wa Kundi D kwa kufikisha alama 04.

Mauaji yamuibua RC Mrindoko
Simba SC yaishusha Al Ahly Afrika