Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa chama hicho hakitashiriki makongamano na vikao vyovyote vya Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) kwakuwa hawaoni ufumbuzi wa kuipata katiba mpya nchini.

Mbowe amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kiini cha tatizo katika nchi i katiba na tatizo la uvurugaji uchaguzi ni Tume ya Uchaguzi.

“Hayo maridhiano yanayozungumzwa kupitia TCD sisi hatushiriki kuyaandaa hatuioni nia njema ya kutibu kiu ya watanzania kuhusu katiba, yametoka matangazo mbalimbali kwamba Mbowe ameridhia mimi sijaridhia kwenda kwenye vikao vya TCD” amesema Mbowe.

”Kuna tetesi kwamba Mbowe ameenda Ikulu amekubali kwamba katiba isiwepo nani kasema maneno hayo? Chadema na katiba hutotutenganisha katiba ndiyo ajenda yetu kuu na tutaipigania siku zote” amesema mbowe

Hata hivyo Mbowe amesema kuwa hana kinyongo na yeyote na Chadema iko tayari kufanya mazungumzo na mtu yeyote, Chama chochote na mashirika ili kuipata haki wanayoitafuta.

Itakumbukwa Machi 17, 2022 kamati ya Chadema ilikutana kujadili mambo kadhaa ikiwemo hatma ya wananchama 19 waliokata rufaa baada ya kufukuzwa uanachama, na kupokea ruzuku za serikali na katiba mpya.

Mpango wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kutekelezwa
Mauaji yamuibua RC Mrindoko