Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ameuagiza Uongozi wa Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu na kuwashughulikia wahalifu wote watakaobainika.

Naibu Waziri Sagini ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa cheo cha Koplo wa Polisi katika Shule ya Polisi iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo jumla ya askari 1750 wamehitimu mafunzo hayo.

Aidha amewataka askari Polisi kote nchini kuendelea kutumia weledi, maadili na ushirikishwaji wa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Sambamba na hayo yote Naibu Waziri Sagini amewaagiza askari hao kwenda kuyashughulikia makosa ya uhalifu wa kimtandao ambapo baadhi yamekuwa yakidhalilisha Utu, Kuchochea chuki na uhasama katika Jamii zetu pamoja na kuathiri uchumi na kutishia amani, utulivu na usalama.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 19, 2022
Mpango wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kutekelezwa