Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara, imeahirishwa leo Machi 22, 2022 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa upelelezi bado haujakamilika, huku ikiwa ni mara ya sita kesi hiyo kuhairishwa tangu kutajwa kwake.

Washitakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele na kutumia dakika 2 tu Mahakamani hapo kabla ya kuahirisha hadi Aprili 5, 2022

Wakili wa Serikali Gidion Magesa ameieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo, kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena.

Aidha kesi hiyo  inawakabili maofisa saba wa polisi ambao ni Ofisa Upelelezi Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje,  Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa zahanati ya Polisi, Marco Mbuta.

Mbwana Makata Kocha mpya Mbeya Kwanza FC
Hitimana: Young Africans bingwa 2021/22