Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Ndugu Saidi Yakubu amesema Wizara Kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linajipanga kuandaa Tamasha kubwa la Muziki wa Taarabu nchini.
Ndugu Yakubu amesema hayo Machi 2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo kilichofanyika Machi 21 na 22 jijini hapo.
“Nawasisitiza tutekeleze majukumu yetu Kwa ufasa na weledi, huku tukitekeleza maelekezo ya viongozi tuweze kufikia Malengo na matarajio ya Serikali” Amesisitiza Ndugu Yakubu.
Katika Baraza hilo mada mbalimbali zimewasilishwa ikwemo Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2021/22 na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2022/23.
Pia Yakubu ametumia muda huo kuwaeleza wajumbe kuwa milango ya Menejimenti ya Wizara ipo wazi na kuwataka kuonana na viongozi wakati wowote wanapokuwa na suala lolote la kikazi ili kuongeza ufanisi wa mahali pa kazi.