Rais wa Jamhutri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya serikali kwa wakazi wa magomeni kota kuwa wapangaji wanunuzi na gharama za ujenzi ujenzi wa nyumba pekee, huku akisisitiza utaratibu katika kusimamia suala hilo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 23, 2022 katika hafla ya ufunguzi wa nyumba 644 za waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota Kinondoni.
“Nimeridhia wananchi hawa kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi na kurejesha gharama za ujenzi pekee, hatutawatoza gharama za ardhi kwasababu tukifanya hivyo mtashindwa,” Amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia amewaasa wananchi hao kuanza kulipa fedha polepole ili Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapate fedha za kumalizia palipo bakia.
“Mnaweza kuanza kulipa sasa na mkianza wote kulipa sasa itakuwa vizuri zaidi kwasababu mtawasaidia TBA wakusanye fedha ya kumalizia eneo lililobakia kwaiyo niwaombe sana muanze kulipa sasa,” Amesema Rais Samia.
Mradi wa magomeni kota ulianza mwaka 2016 katika awamu ya tano chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 52 ambapo kila jengo linabeba kaya 128.