Hatimaye Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva amekanusha taarifa za kuwa mbioni kurejea katika Soka la Bongo huku akihusishwa na klabu nguli za Simba SC na Young Africans.

Msuva aliingia kwenye fununu za usajili wa klabu hizo kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kufuatia sakata lake la kimaslahi dhidi ya Uongozi wa Wydad Casablanca ya Morocco, hali ambayo inatazamwa huenda ikavunja mkataba wa pande hizo mbili.

Baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati uliochezwa jana Jumatano (Machi 24) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Kiungo huyo alizungumza na Waandishi wa Habari na kusema hafikirii kujiunga na klabu za Tanzania na badala yake amejikita kwenye wazo la kuendelea kucheza soka nje ya nchi.

“Kuna klabu nyingi zimeshaonyesha nia ya kutaka kunisajili katika kipindi hiki, lakini sina budi kusubiri hadi sakata langu la Wydad litakapokwisha.”

“Kwa Tanzania hapana.” amesema Msuva

Tayari Shirikisho la Soka Dunia FIFA limeshapokea malalamiko ya Simon Msuva dhidi ya Wydad Casablanca, na wakati wowote maamuzi ya kesi hiyo yatatangazwa.

Bernard Mwalala aitosa Coastal Union
Simon Msuva awatoa hofu watanzania