Bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu amewataka Majaji na Mwamuzi watakaosimamia pambano lake dhidi ya Twaha Kiduku kesho Jumamosi (Machi 26), kutenda haki ili mshindi wakweli apatikane na Dunia ikubali ameshinda.

Twaha Kassim ‘Kiduku’ aliyekua kimya kwa zaidi ya miezi sita, kesho Jumamosi atarejea tena Ulingoni kupapatuana na Kabangu katika pambano lisilokua na Ubingwa ambalo limepachikwa jina kwaa kuitwa ‘MFALME KWENYE UFALME WAKE’.

Kabangu ambaye anaishi Afrika Kusini amesema amejiandaa vizuri kumkabili Twaha Kiduku na anaamini atafanikiwa kutimiza lengo lake la kumpa upinzani wa kweli.

Amesema amekuja Tanzania akiamini ni nchi inayopenda Amani na kutenda Haki, hivyo Majaji na Mwamuzi watakaosimamia pambano lake dhidi ya Mwenyeji Twaha Kiduku wasipindishe ukweli.

“Nimekuaja Tanzania kwa sababu nchi hii ni nchi yangu ya pili baada ya nyumbani kwetu DR Congo, kwa sababu nimewahi kutemba katika baadhi ya nchi za Afrika, lakini nimekua na marafiki wengi hapa.”

“Ninaamini Tanzania ni nchi inayopenda Amani na Haki, hivyo Majaji na Mwamuzi wanapaswa kutenda haki, iwe kwangu ama kwa mwenzangu, atakayeshinda atangazwe kashinda kihalali, haitapendeza pambano likamalizika kwa mmoja kulalamika eti kaonewa.” Amesema Kabangu.

Twaha Kiduku: Nipo tayari, Sitawaangusha
Simba SC yaiweka kando Ligi Kuu, ASFC