Mwanamuziki wa kike mahiri wa Bongo fleva, Faustina Mfinanga maarufu ‘Nandy’ ameweka wazi mfumo wa maisha anayoishi yeye na mchumba wake rapa Billnas.

Nandy amezikataa fununu za kuwa wawili hao wanaishi pamoja kwa kusema kuwa licha ya kuwa wachumba lakini mpaka sasa kila mmoja bado anaishi kwake na kwamba kila wakati huwa wakitembeleana.

“Hatuishi pamoja na Billnass lakini huwa anakuja kulala kwangu na mimi nalala kwake huo ndio utaratibu na tayari ameshalipa mahari”  alisema Nandy.

Aidha licha ya kubainisha hilo Nandy amedokeza kuhusu mwezi ambao wawili hao wanatarajia kufunga pingu za maisha huku akitaja orodha ya sherehe zitakazofanyika kusindikiza hafla ya ndoa yao.

“Kabla ya harusi kutakuwa na sendoff, kitchen party, reception, usiku wa vyombo na singo. Wapare hatuna shughuli ndogo, harusi yangu itakuwa mwezi wa Sita” alisema.

Nandy ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano maalumu kupitia kipindi cha leo tena kinachorushwa na Cloudsfm.

Ali Kiba na Diamond kutumbuiza jukwaa moja
Profesa Ngowi aacha simanzi