Katibu Mkuu wizara ya utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas ametoa ametoa wito kwa Taasisi ya Hakimili Tanzania COSOTA kuendelea kutoa Elimu zaidi kuhusian na hakimiliki, huku akiwasisitiza wahahri wa vyombo vya habari kutumia uwanda Mpana walionao katika habari Ili kufikisha Elimu ya hakimiliki kwa ufasaha.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo ya siku moja ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari huku akisema dhana nzima ya hakimiliki ni kulinda ubunifu wa wahusika katika hakimiliki na hakishiriki.

Aidha amewaasa Watanzania kutumia ubunifu wao vizuri na kuulinda kisheria ili waweze kunufaika kiuchumi

“Kwenye nchi zilizoendelea Hakimiliki imekuwa sehemu kubwa sana ya kipato na sehemu ya kuboresha maisha ya watu na kuongeza chachu ya watu kuendelea kubuni vitu mbalimbali ambavyo pia huingia kwenye ushindani”. Amesema Dkt.Abbasi.

Dkt.Abbasi amesema Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja wametimiza wajibu wake kwa kuendelea kuboresha mazingira mbalimbali ya kusaidia watanzania kunufaika, huku akielezea kuhusiana na mirabaha ambapo amesema kuwa serikali itaan,a kutoa mirabaha kwa wabunifu Kila baada ya miezi sita, ambapo zoezi utarajiwa kuanza mwezi wa saba

Aidha Dkt.Abbasi amesema Serikali imeongeza fedha za usimamizi na uendeshaji wa masuala ya taasisi ya COSOTA ili nao wakusanye fedha na wanaopaswa kupata fedha zao wapatiwe.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi.Doreen Sinare amesema COSOTA imeweza kulipa Mirabaha kwa Wasanii 1,123 ambapo kwa mara ya kwanza na hii ni idadi kubwa, tangu kuanzishwa kwa COSOTA

Amesema jumla ya kazi 5,924 ambazo ni nyimbo za wasanii zilizotumika katika vituo vya redio saba zilitumika kama sampuli kufanya mgao wa mirabaha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akifungua Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA leo Jijini Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Bi.Doreen Sinare akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Angella Mang’enya akizungumza katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatilia Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari katika Mafunzo ya Hakimiliki kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na COSOTA Jijini Dar es Salaam.

Serikali yaweka jicho Upatikanaji wa dawa
Serikali kuboresha ununuzi wa dawa MSD