Kocha Mkuu wa Mafunzo FC ya Zanzibar Said Omar amesema kikosi chake kipo tayari kucheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans.

Mafunzo FC itacheza dhidi ya Young Africans leo Jumatano (Machi 30), Uwanja Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuziandaa timu hizo ambazo bado zinapambana katika Ligi msimu huu.

Kocha Said amesema baada ya kuwasili jijini Dar es salaam jana Jumanne (Machi 29), kikosi chake kilijifua kwa muda mchache Uwanja wa Uhuru na leo Jumatano kipo tayari kupambana na WANANCHI.

“Kwa bahati nzuri mchezo huu umekuja wakati ambao bado tupo kwenye Ligi Kuu ya Zanzibar, hata kwa wenzetu wapo kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hivyo ninaamini timu zitaonyeshana uwezo mkubwa wa kupambana wakati wote,”

“Nafahamu ni mchezo wa Kirafiki, lakini kwangu itakua kama vita kwa sababu lengo langu ni kutaka wachezaji wangu wapambane na wajifunze kitu kutokwa kwa Young Africans ambayo msimu huu ipo vizuri.” amesema Said Omar Kocha wa Mafunzo FC.

Young Africans watautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya kuikabili Azam FC katika mpambano wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa April 06, Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Jumatatu (Machi 28) Azam FC ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB FC inayoshirtiki Ligi Daraja la Kwanza msimu huu, katika Uwanja wa Azam Complex.

Azam FC ilichomoza na ushindi wa 1-0, bao likifungwa na beki wa pembeni Edward Cherles Manyama dakika ya 80.

Bumbuli: Tumeialika Mafunzo FC kwa sababu maalum
Simba SC yakanusha kumfukuza Kocha Pablo