Beki kutoka nchini Brazil na klabu ya Chelsea ya England Thiago Silva amesema klabu hiyo itapigwa na kitu kizito endapo itashindwa kumbakisha Beki wa Pambeni kutoka Hispania Cesar Azpilicueta mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea FC inatajwa huenda ikaachana na Nahodha Azpilicueta, pamoja na mabeki wengine Andreas Christensen na Antonio Rudiger, ambao wataondoka kama wachezaji huru, kufuatia mikataba yao kuwa ukiongoni.

Silva mwenye umri wa miaka 37, amesisitiza kuondoka kwa Mhispania huyo kutaacha pengo kubwa katika kikosi cha Meneja Thomas Tuchel, ambacho msimu huu kimetwaa ubingwa wa Dunia.

Beki huyo amesema: “Yeye ni kijana wa kuvutia, mtaalamu wa hali ya juu ambaye bila shaka anastahili kuwa hapo alipo na kuvaa kitambaa, ambacho kina maana kubwa kwake.

“Kuna manahodha wa aina tofauti, wapo wanaozungumza zaidi na wengine kimya lakini wana maana kubwa kwa timu.
“Azpilicueta ana vipengele vyote viwili. Ni muhimu sana uwanjani na nje anaikutanisha timu inapobidi kuzungumza na kuweka mambo wazi ili yasiharibike.”

Silva alisaini nyongeza ya mwaka mmoja mwezi Januari, ambao utafikia kikomoa mwishoni mwa msimu ujao wa 2022/23.

Beki huyo mkongwe ameonekana kuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na The Blues akitokea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Van Gaal amuonya Erikten Hag kwenda Man Utd
Urusi yapunguza wanajeshi wake Ukraine