Rais wa Urusi Vladimir Putin na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wamezungumza kwa simu kujadili agizo la Moscow kuhusu Berlin kuipa gesi kwa rubles, badala ya euro au dola.
Taarifa kutoka Ujerumani zimedai, Putin amekubali kwamba malipo yaendelea kwa sasa kwa kutumia moja ya sarafu za Magharibi, na kwamba malipo hayo yatabadilishwa kuwa sarafu ya ruble.
Rais Putin amemueleza Scholz kwamba serikali yake sasa inataka malipo yote yafanyike kwa rubles kutokana na ukweli kwamba, ukiukwaji wa sheria ya kimataifa, imepelekea akiba ya fedha za kigeni ya Benki Kuu ya Urusi izuiliwe na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya –EU.
Amesema kuwa ubadilishaji huo hautasababisha masharti ya kandarasi yenye faida kidogo kwa waagizaji wa bidhaa kutoka Ujerumani.
Ujerumani inategemea Urusi kwa zaidi ya nusu ya usambazaji wake wa gesi, na theluthi moja ya mafuta yake hutoka nje.
Viongozi wa Berlin wamekuwa na shauku ndogo ya kuidhinisha vikwazo vya sekta ya nishati kwa Urusi kuliko baadhi ya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Scholz ameelezea kuwa nishati ya Urusi ni muhimu kwa ustawi wa uchumi wa Ujerumani.