Mamlaka ya Mapato Tanzania (TAR) imeutaarifu umma kuwa katika kipindi cha robo Tatu ya mwaka wa Fedha Julai hadi machi 2021/22 imekusanya sh Trilioni 16. 69 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 93.3 ya lengo la kukusanya sh. trilioni 17.15 ambapo makusanyo hayo ni ongezeko la sh. trilioni 3.1 ukilinganisha na makusanyo ya sh. trilioni 13. 59 kilicho kusanywa kwa kipindi kama hiki mwaka wa fedha 2020/21 ongezeko hili ni ukuaji wa makusanyo ya kodi kwa asilimia 22. 8.
Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa kwa umma kwa mwezi machi 2022 TAR imekusanya trilioni 2.06 kati ya lengo ka kukusanya trilion 1.98 makusanyo haya ni sawa na ufanisi wa asilimia 103.6 na ukuaji wa asilimia 23. 17 ikilinganishwa na mwezi machi 2021 amabapo makusanyo yalikuwa trilioni 1. 67.
Tarifa imesema kuwa makusanyao hayo ni kutokana na utayari wa walipa kodi na kulipa kwa hiari ambapo kumechangia kuimarika kwa mahusiao kati ya TRA na walipa kodi kunakochagizwa na utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya Mahakama pamoja na kushughulikia malalamiko ya walipa kodi kwa wakati.
Hata hivyo TRA imepanga kutekeleza mambo yafuatayo