Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amejivika vazi la kizalendo kwa kuwahimiza Mashabiki wa soka nchini kuwa kitu kimoja kuelekea mchezo wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba SC dhidi ya USGN ya Niger.

Simba SC leo Jumapili (April 03), itakua mwenyeji wa USGN ya Niger katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku ikihitaji alama tatu muhimu ili kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22.

Masau Bwire amewataka Watanzania wanaopenda Michezo kuweka pembeni itikidi zao kisoka na kuwa kitu kimoja ili kuipa nguvu timu ya Simba SC, itakayoliwakilisha tarifa leo Jumapili (April 03), saa nne usiku.

Mdau huyo wa Soka wamewataka Mashabiki kujitokewa kwa wingi Uwanja wa Benjamin Mkapa na kujaza nafasi 35,000 zilizotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.

“Sote wazalendo, tuliozaliwa Tanzania, tunaoipenda nchi yetu, tujitokeze kwa wingi, twende uwanjani tukawashangilie Simba SC, wanaoibeba na kuitangaza nchi katika ulimwengu wa soka, tuhakikishe inashinda”

“Kwa Mkapa hatoki mtu haitoshi, tujipange, tujiandae tuwe na ubora wa kutuwezesha kushinda. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba SC” amesema Masau Bwire

Simba SC inahitaji kushinda dhidi ya USGN ili ifikishe alama 10, zitakazoivusha kwenda Robo Fainali, huku Mshiriki mwingine kutoka Kundi D, katika hatua hiyo akitarajiwa kupatikana baada ya mchezo wa RS Berkane ya Morocco itakayokua nyumbani dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Msimamo wa Kundi D unaonyesha ASEC Mimosas inaongoza ikiwa na alama 09, ikifuatiwa na RS Berkane yenye alama 07 sawa na Simba SC, huku USGN ikiburuza mkia kwa kufikisha alama 05.

Dkt. Mabula: Wanachi washilikishwe maamuzi Baraza la Mawaziri
Mathias Lule: Wachezaji wangu wamejisahau