Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Vicky Ford ameonesha kuridhishwa na utoaji wa huduma jumuishi kwa familia, mama, watoto, vijana na watu wenye ulemavu katika kituo cha afya EngenderHealth Tanzania kilichopo Yombo Jijini Dar es Salaam.

Ford ameyasema hayo leo April 4, 2022 wakati alipofanya ziara katika kituo cha EngenderHealth Tanzania ambacho kinafadhiliwa na Serikali ya Uingereza.

“Nimeridhika na utoaji wa huduma katika kituo hiki hasa baada ya kuongea na akina mama, vijana na watu wenye ulemavu kwa nyakati tofauti maelezo yao kwangu yanaonesha huduma ni nzuri na zinaridhisha,” Amesema Waziri Ford.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha EngenderHealth Tanzania, Dkt. Moke Magoma ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa ufadhili wa baadhi huduma katika kituo hicho na kuahidi kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidi na weledi katika kuwahudumia watanzania wanaotumia kituo hicho.

Baadhi ya akina mama waliokuwa katika kituo hicho kwa ajili ya matibabu na huduma mbalimbali wameomba kuongezewa watumishi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa Pamoja na kujengewa kituo nmumuishi ambacho kitaweza kusaidia upatikanaji wa huduma zote katika eneo moja.

Kituo cha EngenderHealth Tanzania kanafadhiliwa na Serikali ya Uingereza katika huduma za mama, mtoto, vijana na wenye ulemavu hasa wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa watoto. 

Huduma nyingine zinazotolewa kituoni hapo ni pamoja na huduma jumuishi kwa familia, mama, Watoto, vijana na wenye ulemavu.

Waziri Ford yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.    

Will Smith anakiona cha mtemakuni kisa Kofi
Kocha USGN aiombea dua njema Simba SC