Kocha Mkuu Azam FC Abdihamid Moallin amesema licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Young Africans jana Jumatano (April 06), hana budi kupongeza juhudi za wachezaji wake walizozionesha wakati wote wa mchezo huo, uliounguruma Uwanja wa Azam Complex, Chamazi-Dar es salaam.

Azam FC ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-1, huku ikitangulia kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji wake Rodgers Kola, kabla ya Beki wa pembeni wa Young Africans Djuma Shaban hajawasazisha kwa mkwaju wa Penati na Mshambuliaji Fiston Mayele kufunga bao la pili na la ushindi.

Kocha Abdihamid Moallin amesema wachezaji wake walijituma wakati wote wa mchezo huo ambao ulikua mgumu, lakini makosa kadhaa waliyoyafanya yamewaadhibu na kupoteza alama tatu wakiwa nyumbani.

Kocha huyo kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Somalia amesema ni wazi bahati haikuwa kwa Azam FC katika mchezo huo, kwani walicheza kwa umakini mkubwa na walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini walishindwa kufanya hivyo na kujikuta upande wa pili wakibahatika.

“Ni ngumu kucheza na timu yenye uzoefu kama Young Africans, lakini kwa wachezaji wangu wameonyesha walikua tayari kupambana na walipambana kweli, licha ya kupoteza kwa mabao 2-1.”

“Tulikaribia kupata bao la pili baada ya wenzatu kusawazisha kwa Penati, lakini bahati haikuwa kwetu kwa sababu kila hatua tulioipiga ilishindwa kufanikiwa tofauti na wapinznai wetu ambao walicheza na kutumia nafasi walizozipata.” amesema Kocha Abdihamid Moallin

Ushindi dhidi ya Azam FC unaiwezesha Young Africans kufikisha alama 51 baada ya kucheza michezo 19, na kuwaacha Mabingwa Watetezi Simba SC iliyocheza michezo 17 kwa alama 11, huku Azam FC wakisalia na alama 28.

Agrey Morris afunguka vita yake na Mayele
Profesa Makubi asisitiza uchangiaji damu salama