Mwamuzi kutoka nchini Tunisia Haythem Guirat ameteuliwa kuchezesha mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali kati ya Simba SC ya Tanzania dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limemtaja mwamuzi huyo sambamba na wasaidizi wake kutoka nchi za Tunisia na Nigeri.

Mchezo huo pia utakua na matumizi ya ziada ya uamuzi ya kutumia VAR, ambapo maafisa watakaoendesha mtambo huo wanatokea nchini Misri.

Waamuzi wasaidizi ni Khalil Hassani (Tunisia), Samuel Pwadutakam (Nigeria) na Sadom Selmi (Tunisia).

Mwamuzi msaidizi upande wa VAR ni Ahmed Elghandour na Youssef Wahid Youssef wote kutoka nchini Misri.

Simba SC itaanzia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (April 17), huku mchezo wa Mkondo wa pili ukipangwa kuchezwa Afrika Kusini April 24.

Simba SC ilitinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuichapa USGN ya Niger Jumapili (April 03), mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D.

Ushindi huo uliiwezesha Simba SC kufikisha alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku timu hizo zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

UN yaiondoa Russia kwenye Baraza la haki za binadamu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, April 8, 2022