Kocha Mkuu wa RS Berkane ya Morocco Florent Ibenge amesema anaamini Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele atakua Mfungaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Mayele juzi Jumatano (April 06) alifunga bao lake la 11, akiifunga Azam FC katika Uwanja wa Azam complex, Chamazi-Jijini Dar es salaam.

Ibenge ambaye amewahi kufanya kazi na Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo katika klabu ya AS Vita, amesema uwezo na ujasiri wa Mayele ndio kumemfanya aamini mchezaji huyo atamaliza kinara katika orodha ya ufungaji bora.

“Mayele atakuwa mfungaji bora Ligi kuu ya Tanzania bara” amesema Kocha huyo kutoka DR Congo.

Wakati Mayele akiongoza msimamo wa ufungaji Bora Ligi Kuu kwa sasa, mpinzani wake wa Karibu ni Mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo aliyezifumanyia nyavu mara 10 huku George Mpole wa Geita Gold akifunga mabao 09.

Utata wa Abdi Banda, Mtibwa Sugar wakaa kimya
Jay Msangi kuwania kiti cha Urais TPBRC