Will Smith amepigwa marufuku kushiliki katika sherehe za kutoa tuzo za Oscars gala na matukio mengine ya Academy kwa miaka 10 baada ya mwigizaji huyo wa Marekani kumchapa kofi mchekeshaji Chris Rock katika sherehe ya kutoa tuzo za Oscars.

Katika taarifa yake Taasisi inayotoa tuzo za Oscars ilisema kuwa hafla ya 94 ya Oscars “iligubikwa na tabia ilisiyokubalika na ya madhara tuliyoona Bw Smith akiionyesha kwenye jukwaa”.

Smith halikuwa ameomba msamaha kwa matendo yake na kujiuzulu kutoka katika Academy ingawa Mwigizaji huyo alimchapa Rock kwa kufanya mzaha kuhusu kichwa cha mkewe kilichonyolewa upara, ambayo ni matokeo ya hali ya kiafya inayosababisha kupotea kwa nywele inayofahamika kama alopecia.

Chini ya saa moja baadaye, Smith alituzwa tuzo ya mwigizaji bora katika nafasi yake katika “King Richard”, ambapo alicheza kama baba yake wachezaji nyota wa tenisi Venus na Serena Williams.

Taasisi ya Academy Of Motion Picture Arts and Science, ambayo iliandaa sherehe za tuzo, iliketi siku ya Ijumaa kwa njia ya video kujadili hatua ya kinidhamu dhidi ya Smith na katika taarifa yake, ilisema kuwa kumpiga marufuku Smith kunalenga kuwalinda waigizaji na wageni na “kurejesha imani katika taasisi.”

Katika taarifa ya kujiuzulu, Smith alisema alikuwa amesaliti Imani ya taasisi ya Academy na alikuwa amevunjika moyo kutokana na matendo yake na aliahidi kukubali kikamilifu matokeo yoyote ya mwenendo wake.

Kujiuzulu kwake kunamaanisha kuwa hataweza kupiga kura katika kura zijazo za wapiga kura wa Oscars.

Tathmini ya Academy Of Motion Picture Arts and Science juu ya tukio hilo, awali ilikuwa imepangwa kufanyika tarehe 18 Aprili, lakini iliharakishwa baada ya Smith kujiuzulu. 

Ni waigizaji wachache ambao wamewahi kujiuzulu katika academy. Wajumbe wanne – mwandaaji wa filamu Harvey Weinstein, mwigizaji Bill Cosby, mkurugenzi Roman Polanski na mwandaaji wa sinema Adam Kimmel – ambao walishutumiwa kwa madai ya tabia mbaya za kingono , huku mwigizaji Carmine Caridi akifutwa mwaka 2004 kwa kuigiza video za skrini alizopewa. 

Lakini viwango vya maadili vinavyoonyeshwa na taasisi hiyo ya mafunzo ya filamu- vinatoa fursa ya hatua mbali mbali za kinidhamu dhidi ya Smith, kama vile kumuondoa katika sherehe zijazo za tuzo za Oscars , kumnyang’anya uwezo wake wa kupata tuzo au kumpokonya tuzo yake mpya aliyoipata ya Oscar.

Ni tuzo moja pekee ya Oscar ambayo iliwahi kuchukuliwa na taasisi kutoka kwa mshindi ambayo ilikuwa ni Makala inayoitwa “Young Americans” aliyoshinda tuzo ya Makala bora zaidi katika mwaka 1969 lakini ilibainika kuwa haikuwa haikustahili kupata tuzo mwaka ule.

Odemba:Polisi Itoe amri Kajala arudi kwa Harmonize
Habari kubwa kwenye magazeti leo, April 9, 2022