Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sister Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo alioshirikishwa wa “Ekwueme” amefariki dunia jana jioni katika Hospitali moja iliyoko Abuja nchini Nigeria.

Taarifa zinasema Osinachi alifariki dunia jioni ya jana Ijumaa (April 8, 2022) baada ya Kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takribani miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.

Wimbo alioshiriki kuuimba wa “Ekwueme” una watazamaji milioni 71 Youtube. Na nyimbo nyingine maarufu ni kama Nara Ekele akiwa na Mchungaji Paul Enenche.

Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.

Osinachi ameacha mume na watoto wanne.

Wachezaji Young Africans watakiwa kupambana
Urusi imemteua Msimamizi mpya wa vita ya Ukraine