Shirikisho la Soka nchini Brazil ‘CBF’ limejipanga kumshawishi Meneja wa klabu ya Manchester City ya England, Pep Guardiola ili akubali kukinoa kikosi cha timu ya taifa hilo, ambalo linaongoza kwenye viwango vya ubora wa soka Duniani kwa sasa.

‘CBF’ wamejipanga kufanya hivyo, huku wakimuandalia Guardioola ofa nono ambayo itamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni milioni 10 kwa mwaka (Sh bilioni 30 na milioni 228).

Hata hivyo Mpango huo umepangwa kufanywa baada ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazounguruma Qatar, baadae Mwezi Novemba, ambapo mkataba wa Kocha wa sasa wa Timu ya taifa ya Brazil Tite utakua umefikia kikomo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Michezo la The Marca la Hispania, Shirikisho la Soka nchini Brazil limeona Guardiola ndiye mtu sahihi anayetakiwa kuinoa timu yao ya taifa hilo.

“Hatua inayofuata ni (kuinoa) timu ya taifa kama nitapata nafasi hiyo,” alisema Guardiola mwanzoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa kuhusiana na timu ya taifa ya Brazil, Guardiola alisema: “Ni timu nzuri ya taifa. Daima Brazil ni chaguo sahihi. Ilikuwa na itaendelea kuwa.”

Guardiola ana mkataba na Man City hadi 2023 na inawezekana akamaliza miaka yake ya mafanikio klabuni hapo.

Wakati huio huo taarifa zinaeleza kuwa Brazil wakakabiliwa na ushindani kufuatia Shirikisho la Soka la Uholanzi kutajwa kumuwania Guardiola  mwenye miaka 51.

Wabunge wamfuta kazi Waziri Mkuu
Mgosi: Pablo atavunja rekodi Simba SC