Rekodi ya ushindi y Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC inapocheza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam katika michuano ya Kimataifa, imemshtua Kocha Mkuu wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Josef Zinnbauer.
Simba SC itakua mwenyeji wa Orlando Pirates katika mchezo wa Robo Fainali Mkondo wa kwanza utakaopigwa Jumapili (April 17), huku Mashabiki 60,000 wakipewa ruhusa ya kushuhudia mchezo huo kutoka ‘CAF’
Kocha Huyo mzaliwa wa Ujerumani Magharibi ameweka wazi juu ya hofu yao na ubora wa Simba SC inapokuwa katika Uwanja wake wa nyumbani, jambo ambalo linamfanya akiri kuwa wanatarajia kuwa na mchezo mgumu japo yupo tayari kwa mapambano.
Amesema amefuatilia michezo ya Simba SC katika hatua ya Makundi ameona timu hiyo ina rekodi nzuri ya kupata ushindi, tena hucheza kwa kujituma zaidi ili kukamilisha lengo lake mbele ya Mashabiki, ambao wamekua wanaonyesha ushirikiano kwa kufika Uwanjani kwa wingi.
Hata hivyo amesema kwake anaichukulia hali hiyo kama changamoto ya kuanza kujipanga kukabiliana na kila jambo litakalomkabili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (April 17).
“Simba katika hatua ya makundi wamepata ushindi katika michezo yao yote ambayo wamecheza nyumbani, rekodi yao pia wanapokuwa katika uwanja wao imekuwa ni nzuri hivyo utaona kabisa mchezo wetu dhidi yao utakavyokuwa.
“Kwetu sisi ni furaha kuona tutapata ushindi dhidi yao pamoja na rekodi na ubora wao lakini pia na sisi tuna upande wetu na sidhani kama itakuwa ni mechi ya upande mmoja pekee, bali ni pande mbili za mapambano haswa ya mpira,” amesema kocha huyo mwenye umri wa miaka 51. Orlando Pirates ilimalzia kinara wa Kundi B kwa kufikisha alama 13 ikifuatiwa na Al Ittihad ya Libya iliyokua na alama 11, huku Simba SC ikimalzia nafasi ya Pili katika msiammo wa Kundi D kwa kufikisha alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, lakini ilimaliza kileleni kwa kuwa na uwiyano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.