Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametahadharisha wafuasi wake kwamba bado wana safari ndefu ya kuibuka na ushindi licha ya kuongoza kwa takribani asilimia 28 katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika April 10, 2022 dhidi ya mpinzani wake mkuu, Marine Le Pen, aliyepata takribani asilimia 23.

Kampeni za duru ya pili zinaanza leo Jumatatu, ambapo Macron anaelekea katika eneo la kaskazini mwa Ufaransa linalokabiliwa na hali mbaya kiuchumi karibu na ngome ya kisiasa ya mpinzani wake ya Henin-Beaumont ambapo wapiga kura wengi walimchangua Le Pen.

Maafisa wa kampeni wa Le Pen wanakutana leo ili kupanga mikakati juu ya duru ya pili ya uchaguzi iliyopangwa kufanyika Aprili 24.

Viongozi hao wawili wamewahi kukabiliana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais miaka mitano iliyopita, japo kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuwa bado Le Pen ana nafasi ya kuibuka na ushindi.

Madiwani Manispaa ya Moshi wamuondoa Meya Raibu
Mangungu, Dalali, Kaduguda kuongoza kampeni Simba SC