Kiungo Mshambuliaji wa Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Lambart Sabiyanka amesema anaamini kikosi cha klabu hiyo kitapmbana hadi mwisho ili kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tanzania Prisons ina wakati mgumu katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikiwa nafasi za chini katika msimamo baada ya kucheza 19 hadi sasa.

Sabiyanka amesema bado wachezaji wa klabu hiyo wana uhakika wa kuibakisha timu yao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao licha ya kuendeleaa kuwa mkiani mwa msimamo.

Amesema wao kama wachezaji wana jukumu la kuhakikisha wanaipambania nembo ya Tanzania Prisons ambapo msimu huu wanapitia kipindi kigumu.

“Ligi imekuwa na ushindani wa hali ya juu, kila timu imejipanga vizuri, na sisi tunapambana kwa nguvu zote kama tulivyofanya mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji na kupata alama tatu.” amesema Sabiyanka.

Tanzania Prisons ipo nafasi ya 15 katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 16, huku Mbeya Kwanza inayoshiriki kwa mara kwanza Ligi kuu ikiburuza mkia ikiwa na alama 14.

Klabu nyingine zilizo kwenye nafasi mbaya na huenda zikakumbana na janga la kushuka daraja msimu huu ni Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji FC.

Mimba zangu nne zilitoka kwa mikosi, ila sasa nina watoto wawili
Opec: Hakuna mbadala wa mafuta ya urusi