Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amekanusha taarifa za Klabu hiyo kuwa mbioni kumsajili Beki wa kati wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Joash Onyango Achieng.

Mapema leo Alhamis (April 14) Young Africans ilianza kuhusishwa na taarifa za kumuwania Beki huyo kutoka nchini Kenya, kufuatia mkataba wake na Simba SC kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Manara amesema taarifa hizo sio za kweli, na Uongozi wa Young Africans umeshangazwa kuona zilivyosambazwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema Klabu ya Young Africans haina mpango wa kumsajili mchezaji yoyote kutoka Simba SC, kwani harakati hizo zimeshapitwa na wakati upande wa klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Hata hivyo Manara amekiri kuwa, Onyango ni Beki mzuri na ameonyesha uwezo mkubwa tangu alipoanza kucheza Soka la Bongo akiwa na Simba SC msimu uliopita 2020/21.

“Sio kweli. Young Africans tushavuka huko, hatutasajili mchezaji yoyote toka huko (Simba). Kweli (Onyango) ni beki mzuri lakini Yanga inafikiria mbali zaidi” amesema Manara.

Kenya, Zimbawe zajumuishwa CAF
Dismas Ten atupia neno usajili wa Onyango Young Africans