Meneja wa FC Barcelona Xavi Hernandez amesema kikosi chake kimepata hamasa baada ya kuhisi maumivu na hasira ya kuangalia michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kikiwa nyumbani.

FC Barcelona inarejea dimbani leo Alhamis (April 14) kwenye mchezo wake wa Europa League ikiwa ni mchezo wao wa pili wa robo fainali, baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya 1-1 nchini ujerumani, na leo usiku wanawakaribisha Frankfurt kwenye dimba la Camp Nuo.

“Tulikuwa tunataka tushinde ligi ya mabingwa lakini tumengukia huku, hii ni tofauti michuano tofauti, japo klabu bingwa inathamani kubwa lakini hata hii ni michuano ya ulaya tutafanya juhudi ili kuweza kushinda.

“Tunafanya kazi kubwa ili kuweza kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya, tumepata hamasa baada ya kuangalia michuano hiyo tukiwa nyumbani, hasira na maumivu ndiyo yataturejesha kwenye michuano hiyo.”

Xavi pia aliongezea kuwa kufanya vizuri kwa klabu ya Real Madrid hakumpi hamasa yoyote kwa sababu klabu ya Barcelona ina historia yake tofauti, na yeye hajui chochote kuhusu Madrid wala hajawai kukaa huko kwahiyo yeye anaendeleza falsafa za Barcelona zilizoanzishwa na Johan Cryuff.

Wahudumu wa afya watakiwa kuzingatia miongozo ya ubora
Kenya, Zimbawe zajumuishwa CAF