Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemtaka Mtanzania mbunifu Masoud Kipanya kufika katika ofisi za shirika hilo na gari la kutumia umeme alilolibuni hivi karibuni ili liweze kukaguliwa na baadaye aweze kupata leseni na cheti cha ubora wa viwango.

Wito huo umetolewa Meneja wa Viwango TBS, Yona Afrika wakati walipotembelea karakana ya mbunifu Masoud Kipanya SIDO ili kuona ubunifu alioufanya kwa kutengeneza gari la kutumia umeme.

Yona amesema wameangalia kwenye maktaba ya kitaifa wakajihakikishia viwango vya upimaji wa magari ya umeme vipo na ndivyo ambavyo watavitumia kukagua gari hilo la kisasa ili kuona hatua ya mwisho ya kupewa leseni ya ubora wa gari linalotumia umeme Tanzania inatoka.

Amri Kiemba: Tatizo liko wapi Simba SC kushinda nyumbani
Rihanna na Asap Roky wameachana?