Meneja wa Beki wa kati wa Young Africans Bakari Nondo Mwamnyeto, amefichua siri ya mchezaji wake kusakwa na Viongozi wa Simba SC ili akubali kujiunga na klabu hiyo ya Msimbazi mwishoni mwa msimu huu.

Mwamnyeto anahusihwa na mpango wa kuwaniwa na Simba SC kufuatia mkataba wake na Young Africans kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa hakuna mazungumzo yoyote huko Jangwani.

Meneja wa beki huyo Kassa Mussa amezungumza na Gazeti la Mwanaspoti na kukiri suala hilo la Viongozi wa Simba SC kumsumbua mteja wake, ambaye kwa sasa bado ana jukumu zito la kuisaidia Young Africans kukata kiu ya Ubingwa wa Tanzania Bara.

“Simba SC wanasumbua sana nisiseme uongo, wamekuwa wakiibuka na ofa kubwa kubwa.. ofa yao ni kubwa hasa ambayo nayo tumeamua kuichukua na kuendelea kuifanyia kazi.” Amesema Kassa.

Hata hivyo Meneja huyo wa Mwanyeto amesema amepokea ofa zaidi ya moja zinazomlenga mchezaji wake, huku moja ya ofa hizo ikitoka kwenye klabu ya nchini Uguriki ambayo hakutaka kuitaja.

“Ukiacha Simba, Bakari ana ofa nyingi sana, kuna ofa tatu au nne hivi, kuna klabu ya Ugiriki, Malta na nyingine moja bado tunazungumza nazo.” Amesema.

Bakari Mwamnyeto alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Coastal Union ya Jijini Tanga, huku akitajwa kuwa beki aliyesajiliwa kwa pesa ndefu zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara hadi sasa.

Ahmed Ally arudisha shukurani kwa Mashabiki Simba SC
Kocha Dodoma Jiji akubali moto wa Mtibwa Sugar