Mmoja wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye alimpatia dawa kijana aliyemuuzia marehemu mwanamuziki Mac Miller vidonge vya fentanyl-laced amehukumiwa kifungo cha miaka gerezani.
Ryan Reavis atakuwa gerezani kwa takriban miaka 10 na miezi 11 baada ya kukutwa na hatia kwa kukiri kumuuzia dawa hizo zilizosababisha umauti wa Miller mapema mwaka jana.
Adhabu hiyo ni ndefu kuliko ile ambayo Reavis mwenyewe aliiomba mahakama impatie, miaka 5 lakini ni fupi kuliko miaka 12.5 ambayo waendesha mashitaka walikuwa wakitaka mtuhumiwa huyo kufungwa.
Inaelezwa kuwa Reavis alitoa tembe hatari za oxycodone kwa anayedaiwa kuwa muuzaji wa madawa ya kulevya wa Mac, Cameron Pettit, kwa maagizo kutoka kwa Stephen Walter, ambaye pia hivi majuzi alikiri kosa la kusambaza fentanyl. Reavis yeye aliweka wazi mbele ya mahakama kuwa alikuwaa mtu wa kati katika biashara hiyo.
Reavis alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 huko Arizona ambapo wachunguzi wanasema walipata daftari la uwongo la daktari, Pia walidai walipata bunduki na dawa za kulevya, ikiwa ni pamoja na vifurushi vya bangi.
Hukumu hiyo ya awali ameipata Reavis anakuwa ni mtu wa kwanza kati ya wanaume watatu walioshtakiwa katika kesi hiyo.
Walter (anayedaiwa kuwa alikimbia) na alitiwa mbaroni licha ya kuwa bado hajajua hatma yake rasmi, mwingine ni Pettit (anayedaiwa kuwa mfanyabiashara na msambazaji) ambaye kesi yake bado haijashughulikiwa.