Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyo husisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika  barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameseama ajaili hiyo imetokea tarehe 19.04.2022 muda wa saa nne usiku na  kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu  na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiri waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.

Rommy 3D:Tumepitia magumu katika Ndoa hii na Shilole
Ahmed Ally amkebehi Manara, ampongeza Thabit Zakaria